Zana ya Earth Defenders: Jinsi ya Kuanza

Ni kitu gani maalum kuhusu mahali unapoishi? Je ni ardhi unayoipenda? Tunakisia kuwa uko hapa kwa sababu kuna sehemu fulani ambayo ni muhimu kwako ambayo ungependa kusaidia kulinda - inaweza kuwa ni mto unaoishi kando kando nao, au msitu ambao familia yako imeishi kwa vizazi vingi. Na, kwa bahati mbaya, ardhi zetu zinazidi kuhatarishwa. 

Zana hii tumeiuunda ili kusaidia watu wanaofanya kazi muhimu ya kulinda dunia -- hasa wale wanaopenda kutumia ramani, ufuatiliaji au zana ya simulizi za hadithi ili kusaidia kulinda ardhi dhidi ya uharibifu wa mazingira. 

Yafuatayo ni baadhi ya maswali na mazoezi ambayo tumeona yanafaa wakati wa hatua za awali za kujenga mradi.

Anzia hapo ulipo

1. Ni nini kinaifanya ardhi/mito/milima/msitu wako kustahili kulindwa?

2. Je, ni matishio gani makubwa zaidi kwenye ardhi yako, na jamii yako?

3. Je, unauwezo wa kufanya mazungumzo na watu wengine katika jamii yako yako ili kuzungumza na kupitia maswali haya na kuorodhesha baadhi ya mawazo yatakayopatikana? 

Zoezi: Mpango wa maisha

Zoezi moja rahisi la kukusaidia kuanza limechochewa na mbinu ya "mpango wa maisha" (plan de vida) ilianzishwa na jamii za Wenyeji nchini Kolombia. Mpango huu unalenga kupata mitazamo kutoka kwa vizazi vyote -- ikiwa ni pamoja na maoni ya wazee, watoa maamuzi pamoja na vijana. Mpango huu unaweza kufanywa na vikundi vikubwa au vidogo, kwa kuhakikisha uwepo wa maoni tofauti kwenye jamill. 

Chukua karatasi tatu kubwa na chora ramani ya eneo lako kwenye kila moja. 

1. Katika ramani ya kwanza, uliza: Eneo la zamani lilikuwa na sura gani? Jadili na chora kama kikundi. 

2. Katika ramani ya pili, uliza: Je, eneo linafananaje leo? Jadili na chora kama kikundi. 

3. Katika ramani ya tatu, uliza: Tungependa eneo liweje kesho? Jadili na chora kama kikundi. 

Kufanya zoezi hili kunaweza kukusaidia wewe na jamii yako kufikiria ni wapi mnataka kuelekeza nguvu zenu.

Ushirikikishaji ni jambo la Muhimu

Neno ambalo unaweza kulisikia sana ni ushirikishi - hii inarejelea miradi ambayo imejengwa kwa njia inayohusisha jamii nzima. Ingawa uchoraji ramani wa kitamaduni unaweza kuhusisha watu wachache tu, katika uchoraji shirikishi kila mtu (ikiwa ni pamoja na vijana na wazee) anahusika katika mchakato wa kutengeneza ramani. Msisitizo huu wa kushirikisha jamii nzima husaidia kuboresha ubora wa ramani na kuhakikisha kuwa inawakilisha mitazamo mingi ndani ya jamii. Eneo la ramani kamwe halipaswi kusemwa na mtu mmoja. 

Maswali ya kuuliza unapoanza

NiniJe, unajaribu kufikia lengo gani? (Mafanikio yangekuwaje?)
Je, unahitaji kukusanya data ya aina gani?
Ni aina gani ya usaidizi wa nje unaweza kuhitajika? (Kama vile kiufundi, kifedha, kisayansi, kisheria, upatikanaji wa zana, mafunzo, n.k.)
Je, ni aina gani ya kazi/shughuli zitakusaidia kutimiza lengo lako? (Kama vile mikutano, mafunzo, kazi ya shambani, ukusanyaji wa data, n.k)
NiJe, ni nani ataathiriwa na mradi huu? 
Nani atashiriki?
Nani ataongoza mradi huu na kuuweka sawa?
Jukumu lako ni lipi?
Nani anaweza kusaidia kazi? (Je, wewe ni sehemu ya shirika au shirikisho linaloweza kuchangia wakati au rasilimali?) 
Je, ungependa kufanya maamuzi vipi kama kikundi?
WapiJe, mradi huu utafanyika wapi?
Je, ni baadhi ya vipengele gani mahususi vya mahali hapa ambavyo vitaathiri mradi? Kama vile muktadha wa kisiasa, shughuli za jumuiya zilizo karibu, n.k.
LiniJe, ni lini unatarajia kukamilisha mradi huu? (Hata kama unatarajia kuwa kazi kubwa zaidi itakuwa ikiendelea, ni vyema kuweka tarehe lengwa ili kutimiza malengo mahususi na kuhakikisha kuwa mradi unaendelea)
KwaNini ni hili jambo ni la maana?
Ni kitu gani kipo hatarini?

Teknolojia

Teknolojia -- kama vile simuza mikononi, ndege zisizo na rubani, kompyuta na GPS -- pekee haziwezi kulinda ardhi zetu. Tulichojifunza ni kwamba teknolojia inakuwa bora zaidi pale inapojumuishwa katika miundo iliyopo kwa ushirikiano ndani ya jamii. 

Teknolojia inaweza kusaidia wakati:

  • unajua ni vitisho gani ungependa kuvielezea, au ni data gani unayotaka kukusanya 
  • unataka kuunda bidhaa mahususi (kama vile ramani, tovuti, kampeni ya utetezi au makala) ambayo aina mahususi ya teknolojia itaweza kukusaidia kuunda.

Teknolojia inaweza pia kuleta matokeo yasiyotarajiwa, na ikiwa unatumia teknolojia kukusanya taarifa nyeti, ni muhimu kuchagua zana zinazowezesha jumuiya yako kudhibiti data zako mwenyewe, ili kuhakikisha kwamba haikuweki wewe au watu wako hatarini kimakosa.

Athari chanya zinazowezekana

  • Kuleta muungano katika jamii katika vizazi vyote. 
  • Kuongeza ushirikishwaji wa vijana katika ulinzi wa ardhi yao. 
  • Kuijenga jamii kupitia mafunzo na ushirikishaji wa kutumia zana
  • Njia bora ya kushirikishana na kuhabarishana data ndani na nje ya eneo husika

Athari hasi zinazoweza kutokea

  • Mabadiliko yasiyotarajiwa katika mienendo ya nishati ya ndani
  • Teknolojia nyingi za kisasa za kidijitali zimeundwa kuwa na uraibu, na kusababisha athari kwa watu binafsi na jamii
  • Katika jumuiya zenye mfiduo mdogo wa teknolojia, uanzishaji wa zana unaweza kusababisha mvutano ndani ya jamii, na kupunguza hadhi ya washiriki kupata zana
  • Huku programu za mitandao ya kijamii kama Facebook, WhatsApp na Instagram inaweza kuwa muhimu katika kuunganisha jumuiya, inaweza pia kuwa na madhara, na kuvuruga desturi za kijamii zinazostawi
  • Kupunguza wajibu na majukumu ya wazee katika jamii ikiwemo na kupunguza ujuzi wa kitamaduni walionao

Baadhi ya mambo ambayo tumejifunza 

  • Ni sawa ikiwa hujui hasa kile unachofanya unapoanza! Katika uzoefu wetu, kila mradi uliofanikiwa hubadilika kwa wakati.
  • Kujenga uaminifu ni muhimu.
  • Furahia!!
  • Kila mtu hufanya makosa - ni sawa kujifunza unapoendelea.
  • Jifunze kutokana na uzoefu wa jumuiya nyingine!